Thank you Joan for your brilliant translation of Mama Junior’s email. Below is my response, in Kiswahili!. Apologies to those who can’t understand it; a translation shall follow shortly.
Habari shaangazi,
Asante kwa kunitumia hio barua ya komputer, ijapokua hiyo lugha ya Kikuyu ilinipa shida kidogo.
Nimeshangaa kusoma ati siku hizi wajiita Mama Junior na sisi sote tunajua hauna mtoto anayeitwa Junior. Naelewa hii mambo ya kuishi ngambo. Nimeona hiyo kipindi inatiwa “Jerry Springer� na nina jua kwamba kuna watu waneweka siri miaka mingi halafu wanakuja kuitoboa kwenye TV. Kwa hivyo kama unaye mototo uliomficha hizo miaka zote; si neno tutamkaribisha tu kwa hii familia yetu. Bora asiwe ni pesa tu anatafuta na asiwe mtu mfupi sana.
Nimefurahi kusoma ati mimi ni mschana mrembo; asante. Unajua wewe piya ni mama poa sana, ijapokoa miaka zimezidi kidogo, wewe bado manyanga..
Kuhusu pombe usijali. Hakuna wakati utasikia nimelala cell au nimekutwa na polisi barabarani usiku za manane nikiimba “Jumbe nipeleke kwetu…�
Sita enda kupotela huko Belize lakini pia ukumbuke mtu hawezi kuitwa bwana kama ngombe hazijafika boma ya baba. Tafadhali harakisha huyu mzee wangu kidogo. Kabla ni rudi ningependa kusikia kwamba mzee wangu ashampelekea baba ka-something. Itisha
- kondoo (hawana mbuzi hapa!),
- kuku (zakutega mayayi),
- jogoo (yaani baba ya hizo mayayi)
- vifranga (hizi tutalea ndio tupate nyama kama ya Kenchic)
- BMW, nyeusi ile watu huita “7 series� (si mimi niko na degree, kwanza kutoka ngambo, siwezi panda matatu au Metro Shuttle!).
Ngombe za Ulaya sitaki, ziko na kasoro.
Natarajia hii baraua itafika vizuri. Salimia kila mtu.
Ubarikiwe.
Ni mimi
Wangui.