Kui Says: You are a funny one! But hata mimi I had no clue what vidonge meant – I had use an online Kamusi
]]>Wanawake ni wajanja na uerevu wanao,
Waona baba likija wambiwa ni shemejio,
Mwalishwa sahani moja kumbe ni mume mwezio…jomba
[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao
[Bibie]
Kulishwa sahani moja wewe na mume mwenzio,
Usikione kihoja dunia yetu ya leo,
Wake nasi tuna haja ya matumizi na nguo
Wanawake ni wajanja hakika nimekubali,
Waona baba likija limevaa suruali,
Mwalishwa sahani moja kumbe ni mume wa pili……jomba
[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao
[Bibie]
Kulishwa sahani moja wewe na yule fulani,
Usikione kioja wala usione shani,
Kumbuka nasi ni tu waja tuna mengi twatamani….
Kui Says: Asante sana for that. Any chance of getting a translation?
]]>